Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka viongozi nchini kuachana na tabia ya kujikweza mbele za watu na badala yake kuishi kama binadamu wa kawaida kwani kwa kufanya hivyo hakuwapunguzii cheo walicho nacho.
Amesema watanzania hatutakiwi kubaguana kwa dini wala kabila na kwamba Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ukubwa aliokuwa nao kama Raisi alikuwa mtu wa kawaida mbele ya watu wengine kwa namna alivyokuwa anahusiana na watu hali iliyopelekea mtu akikaa naye hapati hofu ya kwamba amekaa na rais.
Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza katika kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jijini Dar es Salaam.
“Ni jambo la muhimu viongozi kutambua kuwa kujishusha hakukufanyi usiwe kiongozi kwasababu una wakati wa kutimiza majukumu yako lakini unapokuwa na binadamu wenzako wako kama wewe,”.
“Watanzania wenzagu, wanachama wenzangu wa CCM na vyama vingine vya siasa, wa rangi zote, makabila yote na madhehebu yote ya dini tushikamane katika kusimamia tunu hii, amani na umoja hauna kabila wala chama na mtu yeyote anayepuuza mambo haya haitakii mema nchi yetu wala yeye mwenyewe,” amesema Dk. Kikwete.
from MPEKUZI https://ift.tt/2ATMc3a
via IFTTT
No comments:
Post a Comment