Tuesday, September 24, 2019

TECNO Kujiweka Karibu Zaidi Na Wateja Wake.

Kampuni ya simu ya TECNO inayotambulika kwa uzalishaji wa simu za viwango vya hali juu imezidi kutanuwa wigo wa soko la simu nchini Tanzania na hii ni mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la simu za TECNO maarufu kama ‘TECNO Smart Hub’ Kariakoo kwa lengo ikiwa kufikisha huduma sitahiki kwa wateja wake.
Hii ni Smart Hub ya tatu kufunguliwa nchini Tanzania na kampuni ya TECNO. TECNO smart Hub zimekuwa zikijihusisha na uuzaji wa bidhaa za TECNO tu kama vile simu za mkononi, chaji, battery, powerbank, cover za simu lakini pia zinatoa elimu kuhusiana na utumiaji na utuzaji wa simu.

“TECNO Smart Hub itahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja lakini vile vile kwa bidhaa zetu zina warranty ya mwaka mmoja na mwezi mmoja” alisema afisa wa mahusiano wa kampuni ya simu ya TECNO Bwana Eric Mkomoye.

Uzinduzi huo uliambatana na tafrija fupi kutoka kwa mchekeshaji Mpoki Mujuni almaarufu Mpoki, Jsquare dancers, na michezo mingine ikiwepo luck draw kwa wateja walionunua simu ndani ya siku hiyo na kujishindia fridge, TV na zawadi nyengine kibao.

Kwa maelezo mengi zaidi tembelea @tecnosmarthub.



from MPEKUZI https://ift.tt/2mlqtx0
via IFTTT

No comments:

Post a Comment