Tuesday, September 24, 2019

Walimu Mkoani Kagera Watakiwa Kuwa Mabalozi Wazuri Wa a Kulipa Kodi Ili Kukuza Uchumi Wa Nchi.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti  amewataka walimu mkoani humo kuwa mabalozi wazuri kwa kulipa kodi ili kuweza kuchangia ukuaji wa pato la nchi.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti amesema hayo Septemba 23, 2019 wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB Bukoba katika siku ya walimu kwenye ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba .
 
Ameongeza kwamba walimu  ni  jeshi kubwa kila watakapo kuwa wenasimama waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ulipaji kodi na kuwahamasisha wananchi kudai risiti kila wakinunua bidhaa na kuwahamasisha wanaouza kutoa risiti.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti ametoa rai kwa benki ya NMB kuona namna ya kuwapunguzia riba walimu sababu ni wadau wakubwa wa benki hiyo tangu mwanzo.
 
 Pia amewataka walimu kutanua wigo wa kuunda vikundi vya pamoja mfano kwenye Kata na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu. 
 
 Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Gabulanga iliyopo wilayani Missenyi bwana Mutalemwa Makwabe kwa niaba ya Walimu wenzake amesema kuwa wanaishukuru benki hiyo kwa namna inavyoendelea kuwajali walimu pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika shule uku akitaja kuwa shule yake iliwahi kupatiwa misaada mbali mbali na benki hiyo ikiweno madawati pamoja na mbao za kuezekea.

Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya ziwa bwana Ibrahimu Agustino amesema kuwa benki hiyo inatenga 1% kila mwaka katika kuhudumia jamii  na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wametenga shilingi bilioni moja na mpaka sasa wametoa zaidi ya milioni mia sita katika  kusaidia jamii.






from MPEKUZI https://ift.tt/2lkQQD7
via IFTTT

No comments:

Post a Comment