Friday, October 11, 2019

Iran yasema meli yake ya amfuta imeshambuliwa pwani ya Saudia

Makombora mawili yameipiga leo meli ya mafuta ya Iran katika Bahari ya Shamu kwenye pwani ya Saudi Arabia, ikiwa ni tukio la karibuni katika jimbo hilo kufuatia miezi kadhaa ya mivutano mikubwa kati ya Iran na Marekani. 

Saudi Arabia haijatoa taarifa yoyote kuhusu madai ya shambulizi hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  Sayyid Abbas Mousavi amesema uchunguzi uliofanywa na Shirika la Taifa la Mafuta la Iran unaonesha kuwa meli hiyo leo Ijumaa asubuhi imeshambuliwa mara mbili kwenye Bahari Nyekundu katika mashambulizi yaliyopishana kwa takriban nusu saa.

Amesema mafuta yaliyokuwa yanamwagika kwenye meli hiyo yamezuiwa na  hakuna mfanyakazi yeyote wa meli hiyo aliyepata madhara.

Televisheni ya taifa ya Iran imesema mlipuko huo uliharibu vyumba viwili vya meli hiyo na kusababisha kuvuja kwa mafuta katika Bahari ya Shamu karibu na mji wa bandari wa Saudia wa Jiddah. 

Jeshi la wanamaji la Marekani linaloendesha operesheni zake Mashariki ya Kati limesema maafisa wamefahamishwa kuhusu ripoti za tukio hilo, lakini wakakataa kutoa taarifa zaidi. 

Tukio hilo limetokea baada ya Marekani kudai katika miezi ya nyuma kuwa Iran ilizishambulia meli za mafuta karibu na Mlango wa bahari wa Hormuz, katika Ghuba ya Uajemi kitu ambacho Iran ilikanusha.


from MPEKUZI https://ift.tt/32aqV0Q
via IFTTT

No comments:

Post a Comment