Thursday, October 10, 2019

korea kaskazini Yatishia kufanya majaribio ya Makombora Ya kinyuklia

Korea kaskazini imeziita shutuma za mataifa ya kigeni kuhusiana na kufyatua makombora yake kuwa ni uchokozi mkubwa, na kutishia kuanza tena majaribio ya makombora ya masafa marefu ya kinyuklia.

Tahadhari iliyotolewa leo na wizara ya mambo ya kigeni ya Korea kaskazini inafuatia kuvunjika mwishoni mwa juma mazungumzo ya kinyuklia kati ya Korea kaskazini na Marekani nchini Sweden, ya kwanza ya aina hiyo kufanyika kati ya nchi hizo katika muda wa zaidi ya miezi saba. 

Taarifa ya wizara hiyo imechukizwa na hatua ya shutuma zilizotolewa siku ya Jumanne na mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya katika baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuhusiana na majaribio ya makombora na silaha nyingine ya hivi karibuni yaliyofanywa na Korea kaskazini.

Mwaka jana Korea kaskazini ilisitisha kwa muda majaribio ya makombora ya masafa marefu ya kinyuklia, na kuvunja maeneo ya majaribio. 

-DW


from MPEKUZI https://ift.tt/329FUsc
via IFTTT

No comments:

Post a Comment