Thursday, October 3, 2019

Korea Kaskazini Yazindua Kombora Hatari la Majini

Korea kaskazini imethibitisha kufanya jaribio la kurusha aina mpya ya kombora, baada ya kufanikiwa kurusha makombora ya masafa mafupi tangu mwezi Mei.


Jaribio hili nchini humo ni la kumi na moja kwa mwaka huu ambapo makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia yanarushwa.

Lakini utofauti wa jaribio hili ni kuwa, kombora halijarushwa kutoka ardhini, bali kwenye nyambizi chini ya bahari.

Kombora hili kuwa na uwezo wa kurushwa kutoka majini ni muhimu zaidi kwa nchi hiyo kwa kuwa sasa wanauwezo wa kufanya mashambulizi mbali ya eneo lao.

Kwa mujibu wa maofisa wa Korea Kusini, kombora hili lina uwezo wa kuruka kwa kasi ya km 450 na kufika urefu wa km.910 kabla alijashuka baharini.

Hii ina maanisha kuwa makombora haya yana uwezo wa kuruka umbali mrefu mara mbili wa kiwango cha kimataifa ingawa makombora ya awali ya Korea Kaskazini yalikuwa na uwezo wa kuruka mbali zaidi.

Kombora hilo liliangukia baharini upande wa Japani, unaoitwa upande wa mashariki wa bahari.

Japani imedai kuwa kombora hilo limetua katika umbali wa kilimita 200 kutoka ardhi yake. .

Jaribio hilo linakuja muda mfupi baada ya Korea Kusini kusema kuwa mazungumzo ya nyuklia kati yao na Marekani yataendelea.

Makombora hayo yalizinduliwa baharini siku ya Jumatano majira ya saa saba usiku saa za Afrika mashiriki, kilomita 17 kaskazini mashariki mwa fukwe za mji wa Wonsan .

Ripoti kutoka televisheni ya taifa hilo KCNA imesema kuwa leo Alhamisi, majaribio matatu kutoka juu yatarushwa ," makombora haya yamebuniwa kutoa vitisho kwa mataifa mengine na kujilinda".

KNCA imeongeza kuwa hakuna madhara yatayotokea kwa nchi za jirani. 
 
Kama makombora hayo yalizinduliwa kwa kiwango cha kawaida, basi yale yaliyorushwa kwa kunyooka wima yana uwezo wa kusafiri kwa karibu kilomita 1900.

Hivyo masafa hayo yanaweza kuzifikia Japani na Korea Kusini.

Korea Kaskazini ina nyambizi iitwayo 'Romeo' kilijengwa mwaka 1990, na wanaamini kuwa na kasi ya kilomita 7,000 ,Reuters imeripoti.

Nyambizi hiyo ina uwezo wa kufanya safari ya moja kwa moja mpaka kufikia Hawaii, Marekani.

Chombo hicho cha majini kinachotumia nguvu ya mafuta ya dizeli, hata hivyo kinapiga kelele ambazo zinaweza kurahisisha kugundulika kirahisi.

Kuzinduliwa kwa kombora hilo la majini na Korea Kaskazini ni hatua mbaya zaidi kwa usalama wa majirani zake wa ukanda wa kaskazini mashariki mwa Asia.

Kombora hili limezinduliwa kwa mipango ya baadae ya majini lakini uzinduzi huu hauoneshi hilo.

Wataalamu waliounda kombora hilo Korea Kaskazini wanasema kuwa ni hatari sana kufanya operesheni hiyo ya jaribio la kurusha kombora majini.

Ingawa kurushwa kwake kunaonekana kuwa ni mafanikio makubwa.

Kama kombora hilo lingerushwa kama kawaida, yangeweza kufika katika visiwa vikubwa vinne vya Japan na ukanda wote wa Korea Kusini.

Hii inatajwa kuwa mfumo hatari zaidi wa teknolojia ya kombora kutambulishwa katika taifa hilo.


Credit:BBC


from MPEKUZI https://ift.tt/2oFTNPQ
via IFTTT

No comments:

Post a Comment