Tuesday, October 15, 2019

NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

Matokeo ya darasa la saba 2019, yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.

Dk. Msonde amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.

Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi  Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar  es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.

"Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,"


from MPEKUZI https://ift.tt/33zmT2x
via IFTTT

No comments:

Post a Comment