Monday, October 14, 2019

Rais Magufuli amkabidhi Naibu Mkurugenzi wa Takukuru ripoti ya miradi 107 yenye Dosari

Rais   Magufuli amemkabidhi naibu mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti ya miradi 107 iliyobainika kuwa na dosari.

Miradi hiyo ilibainika kuwa na kasoro ilipotembelewa kwa ajili ya kuzinduliwa na kukaguliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofikia kilele chake leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.

Rais Magufuli amekabidhi ripoti hiyo leo katika maadhimisho ya kilele hicho na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika mkoani Lindi.

Awali, kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Mzee Mkongea Ally alimkabidhi Rais Magufuli ripoti ya miradi ya Sh90.28 bilioni iliyokutwa na dosari.

“Sogea hapa mbele nikukabidhi ripoti hii, zege halilali. Naikabidhi hii ripoti ukafanye ukaguzi kila ukurasa, kila nukta na ukachambue wale wote wanaohusika wapelekwe mahakamani. Usisite wapeleke mahakamani,” amesema Rais Magufuli wakati akimkabidhi Brigedia  Jenerali Mbungo ripoti hiyo.


from MPEKUZI https://ift.tt/2VQ1uj7
via IFTTT

No comments:

Post a Comment