Friday, October 4, 2019

Rais Magufuli Atatua mgogoro wa ardhi kati ya Wananchi na kiwanda cha Saruji Mbeya

Rais Magufuli ameagiza wakazi wa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, kuendelea kulitumia eneo lenye ukubwa wa ekari 2,115 linalogombewa na wakazi hao na kiwanda cha Saruji Mbeya.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposimama katika kijiji hicho cha Nanyala na kuelezwa kero hiyo na mwenyekiti wa kijiji hicho, Philemon Namwema.

Mwenyekiti huyo amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli yoyote, wananchi  23 wakikabiliwa na kesi mahakamani.

Akitoa uamuzi huo, Magufuli amewaagiza mawaziri kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo mahakamani na baada ya hapo wamjulishe ili aweze kubadili matumizi ya eneo hilo.


from MPEKUZI https://ift.tt/2LMsWuw
via IFTTT

No comments:

Post a Comment