Thursday, October 10, 2019

Tanzania na Kenya zaongoza kwa idadi ya mabilionea Afrika Mashariki

Kenya na Tanzania zinaongoza kwa idadi ya watu matajiri katika jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na utafiti uliofanywa.

Kwa mujibu wa ripoti ya 2019 kuhusu utajiri barani Afrika iliyochapishwa mwezi Septemba na Benki ya AfrAsia, Kenya inaongoza ikiwa na mabilionea 356, Ikifuatiwa na Tanzania ambayo ina mabilionea 99.  Nchi ya Uganda ni ya tatu ikiwa na matajiri 67 huku Rwanda ikifunga orodha hiyo na mabilionea 30.

Ripoti hiyo inasema kwamba matajiri hao wana utajiri wa dola bilioni 10 na kwamba Tanzania ina tajiri mmoja wa dola bilioni moja.

Barani Afrika ripoti hiyo inasema kwamba Afrika Kusini inaongoza kwa matajiri ikiwa na mabilionea 2,169, Misri 932 na Nigeria 531.

Katika miji mikuu, mji wa Nairobi unaongoza ukiwa na utajiri wa dola bilioni 49 mbele ya mji wa Dar es Salaam ambao umeorodheshwa namba 11 na una utajiri wa dola bilioni 24.

Mji mkuu wa Uganda Kampala una utajiri wa dola bilioni 16 huku Addis Ababa ikiwa na utajiri wa dola bilioni 14.

Kulingana na ripoti hiyo mabilionea wa Afrika ni asilimia 16 pekee ya idadi ya mabilionea wote duniani, huku Afrika ikiwa na asilimia moja pekee ya utajiri wote duniani.

Utajiri unaomilikiwa na bara la Afrika ni dola trilioni 2.2 kwa jumla ambapo asilimia 42 ya utajiri huo unalimikiwa na watu wenye utajiri wa kiwango cha juu.

Ripoti hiyo inasema kwamba kuna matajiri 140,000 wanaoishi barani Afrika kila mmoja wao akiwa na mali yenye thamani ya dola milioni 10.

Credit: BBC


from MPEKUZI https://ift.tt/2IEaa6D
via IFTTT

No comments:

Post a Comment