Tuesday, October 8, 2019

Uturuki: Maandalizi ya kuivamia Syria yalikwishakamilika

Uturuki imesema maandalizi ya kushambulia eneo la kaskazini mwa Syria yalikwishakamilika ikiwa ni baada ya dalili zenye mkanganyiko kutoka Marekani kuhusu iwapo itaruhusu operesheni hiyo ya kijeshi. 

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imeandika kwenye ukurasa wake wa twitter muda mfupi baada ya Marekani kuondoa majeshi yake kwenye eneo la mpaka kwamba maandalizi yote yalikuwa yamekamilika. 

Kuliibuka utata siku ya Jumatatu wakati rais Donald Trump wa Marekani aliposema atauharibu uchumi wa Uturuki iwapo itafanya chochote ambacho hakitampendeza. 

Ankara imesema inataka eneo salama litakalotumiwa dhidi ya vikosi vya Wakurdi na kuruhusu takriban wasyria milioni mbili kurejea nyumbani. 

Katika hatua nyingine rais Trump ametetea uamuzi wake wa kuachana na wanamgambo wa Kikurdi nchini Syria akisema ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya kujiondoa kwenye "vita visivyo na mwisho" huko Mashariki ya Kati.


from MPEKUZI https://ift.tt/2LViOzM
via IFTTT

No comments:

Post a Comment