Friday, October 4, 2019

Walichokisema CHADEMA Kuhusu Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiri kupokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kuhusu Uchaguzi Mkuu wa ndani wa Chama hicho, na kusema Chama hicho hakijakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa Nchini wala Katiba ya Chama.

CHADEMA wamesema Katiba ya Chama hicho, ibara ya 6.3.3 (a) inatoa mamlaka kwa Kamati Kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa ndani ya Chama, na kwamba Mamlaka ya kufanya marekebisho hayo yameachwa kwa Kamati Kuu .

CHADEMA wamesema Kamati Kuu ya Chama ilikaa katika kikao chake cha tarehe 27 na 28, Julai, 2019, na kurekebisha ratiba ya uchaguzi ambapo utakamilika mwezi Disemba kwa ngazi ya Taifa na Katika hatua ya sasa, Chama kinaifanyia kazi barua hiyo ili iweze kuifikia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya muda husika uliotajwa.



from MPEKUZI https://ift.tt/2LLoQTj
via IFTTT

No comments:

Post a Comment