Thursday, October 17, 2019

Waombaji 30,675 Bodi ya Mikopo wapata mkopo elimu ya juu awamu ya kwanza.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  imesema wanafunzi 30,675 kati ya wanafunzi 45, 000 wa mwaka wa kwanza wa masomo 2019/20 walioomba mkopo kwa awamu ya kwanza wamepata.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba  17, 2019, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema jumla ya Sh113 bilioni zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao na fedha ambazo Serikali imeshaikabidhi bodi hiyo  ni Sh125 bilioni.

Amesema kati ya orodha hiyo wanafunzi wa kike ni 11,043 sawa na asilimia 36 na wakiume ni 19,632 sawa na silimia 64.

Hata hivyo,  amesema orodha ya awamu ya pili itatangazwa Oktoba 25,2019 baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udahili na kurekebisha maombi yao ya mkopo mtandaoni.

Amesema fedha za wanafunzi ambao wamefanikiwa kupata mkopo  zitatumwa vyuoni mapema kabla havijafunguliwa.



Tembelea <<HAPA >> Kwa taarifa mbalimbali za Ajira Tanzania , Bodi ya Mikopo(HESLB), Scholarships



from MPEKUZI https://ift.tt/31mg0A0
via IFTTT

No comments:

Post a Comment