Thursday, October 3, 2019

Waziri Jafo Awataka Wakurugenzi Wapya Wajiamini na kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Mhe.Seleman Jafo amewataka Wakurugenzi wapya 10 walioteuliwa hivi Karibuni na Rais Magufuli kujiamini katika nafasi zao na kusimamia mahusiano mema ya Utumishi.
 
Waziri Jafo amesema hayo leo Oktba 3,2019 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi hao Wapya pamoja na Ofisi ya TAMISEMI kilichoenda sambamba na kula kiapo cha utumishi kwa Watumishi hao.
 
Waziri Jafo amesema suala la kujiamini ,kusimamia mahusiano mema pamoja na Maadili ni jambo la msingi kwa kila mtumishi,hivyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kutengeneza manung’huniko ya madaraja katika halmashauri zao.
 
Aidha ,Waziri Jafo amewataka wakurugenzi hao kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo kwani wasipozingatia mambo hayo halmashauri zao zitayumba kutokana na kukosa mapato.
 
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka wakurugenzi kujiheshimu katika kazi zao .
 
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkurungezi ni heshima kubwa ,Itakuwa jambo la ajabu mkurugenzi umeweka miito ya Muziki wa Ovyo,sijui Singeli kwenye simu yako,Sijui mkurungezi ukipanga foleni kwenye chakula sahani ya ubwabwa unaijaza mpaka unamwagika,au unanunua miwa unakula ovyo barabarani.kwa hiyo ukurugenzi ni heshima kubwa.Amesema.
 
Kaimu  katibu Mkuu TAMISEMI,Mathias Kabundugulu  amewataka wakurugenzi hao kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kusimamia vyema uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
 
Ikumbukwe kuwa ,Oktoba Mosi 2019 Rais Wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji 10 wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa na kuwahamisha wawili.


from MPEKUZI https://ift.tt/2oKurjQ
via IFTTT

No comments:

Post a Comment