Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Genelari Marco Elisha Gaguti ameendelea kuwasisitiza wananchi mkoani kagera kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpiga kura ndani ya siku mbili ambazo zimesalia kufikia tarehe 14 mwezi wa 9 mwaka huu ambapo itakuwa ni mwisho wa zoezi hilo.
Akizungumza na wananchi wa kata Kemondo katika mkutano wa hadhara, mkuu wa mkoa wa Kagera amebainisha tofauti iliyopo kati ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ambapo amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lililohusisha pia uboreshaji wa taarifa mbalimbali za wananchi kuwa vitambulisho hivyo vilivyotolewa ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa madiwa,wabunge na Rais.
Brigedia Gaguti amesema kuwa zoezi linaloendelea kwasasa ni kwaajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji, hivyo amewataka wananchi ambao bado hawajajiandikisha kutumia vyema siku hizi mbili kujitokeza nakujiandikisha katika vituo vilivyopo katika maeneo yao.
Sanjari na hayo Brigedia Gaguti ametoa pongezi kwa wananchi na viongozi wa halmashauri ya wilaya Bukoba kwa ushirikiano nakusema kuwa kwataarifa za awali zinazohusu uandikishaji wa wapiga kura zilizotolewa tarehe 11 mwezi huu wilaya ya Bukoba imefanikiwa kwa asilimia 82.4 ambacho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na wilaya za Karagwe,Kyerwa,Misenyi,Mleba,Ngara,Biharamulo pamoja na manisipaa ya Bukoba.
Hata hivyo mkuu wa mkoa amesema viongozi wa ngazi za mitaa na vijiji ndio viongozi muhimu na watakaotumika kuleta maendeleo kutokana na ukaribu wao kwa wananchi katika kufikia uchumi wakati na wa viwanda kama ilivyo azima ya nchi.
from MPEKUZI https://ift.tt/2MAgMEi
via IFTTT
No comments:
Post a Comment