Mkurugenzi wa Kampuni ya SKOL, Vicent Massawe ameishiwa nguvu na kuanguka ghafla baada ya Waziri Jafo kumpa siku 26 kukamilisha Mradi wa Barabara ya Swaswa, Dodoma kwa kiwango cha lami(KM1.8) na kuagiza akishindwa kukamilisha asipewe tena kazi Tamisemi.
Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019.
Kutokana na kuchelewa huko mkandarasi huyo amekatwa Sh80 milioni na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).
Licha ya kujitetea kuwa wamejenga katika miradi mingi nchini ikiwemo katika jimbo la Kisarawe ambalo mbunge wake ni waziri huyo wa Tamisemi, waziri huyo alikataa na kubainisha kuwa uwezo wa kampuni hiyo ni mdogo.
from MPEKUZI https://ift.tt/34RXB0C
via IFTTT
No comments:
Post a Comment