Wednesday, December 4, 2019

RC Kagera Aongoza Wananchi Kufanya Usafi Na Kuchangia Damu Baada ya Kuzindua Maadhimisho Ya Miaka 58 Ya Uhuru

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amezindua rasmi maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kushiriki katika kufanya usafi katika soko kuu la Bukoba na maeneo mbalimbali pamoja na uchangiaji wa damu katika hospital ya rufaa ya Mkoa kagera (GOVERNMENT).

Mara baada ya kushiriki usafi ndani na nje ya Soko Kuu la Bukoba, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliongea na wananchi waliokusanyika kufanya usafi pamoja naye na kuwaeleza maudhui ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaeleza kuwa mwaka huu 2019 maadhimisho hayo yanaadhimishwa Kanda ya Ziwa ambapo mikoa miatano inashiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali.
 
Baada ya hapo Gaguti ameweza kutembelea na kukagua hospital ya rufaa ya mkoa Kagera (government) ambapo ameweza kukagua ujenzi ambao ulikuwa ukiendelea hospitalini hapo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaongoza wananchi na viongozi mbalimbali kuchangia damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo mpaka anaondoka katika eneo hilo tayari chupa 63 zenye ujazo wa nusu lita za damu zilikuwa zimekusanywa malengo yakiwa ni kukusanya chupa 400 kwa siku hiyo tu.

Kwa upande wake kaimu mganga Mfawidhi wa hospital hiyo Msereta Nyamkoroto amesema kuwa kuna jumla ya vitanda 308 na wanapokea wagonjwa 160 kutoka nje ya mkoa ambapo 60 Tu ndio wanatoka ndani na kuongeza kuwa wanawake hasa wajawazito pamoja na watoto chini ya miaka 5 ndio wana matumizi makubwa ya damu ambapo wanawake wanaojifungua kwa siku ni 11 na vifo ni 1 kwa mwezi.

Kilele cha Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni tarehe 9 Desemba 2019 Mkoani Mwanza na Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “Miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri: Uzalendo, Uwajibikajina Ubunifu ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi na Taifa letu.”



from MPEKUZI https://ift.tt/2sMXSDY
via IFTTT

No comments:

Post a Comment