Tuesday, February 16, 2021

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge; Ushawishi Wa Tanzania Bado Ni Imara Kikanda Na Kimataifa


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge amaeleza kuwa nguvu ya ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kikanda na kimataifa bado upo imara, licha ya Tanzania kutoa mchango mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika na uanzishwaji wa Jumuiya za Kikanda kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hadi hivi sasa Tanzania bado ni kinara katika kutetea na kudai maslahi ya Bara la Afrika.

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge, amebainisha haya alipokuwa akizungumza na wadau kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) ambao waliitemebelea Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya Wizara, hasa katika kutetea maslahi ya Nchi nje ya mipaka ya Tanzania. 

Katibu Mkuu aliendelea kubainisha kuwa Wizara katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje pamoja na mambo mengine inahakikisha kuwa inatoa kipaumbele kwenye kulinda maslahi ya Nchi ikiwewo ulinzi na usalama.

NDC kwa upande wao wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanywa na Ofisi zake za Ubalozi sehemu mbalimbali duniani katika kutangaza fursa zilizopo nchini kwenye maeneo yao ya uwakilishi madhalani utalii, biashara ya madini na mazao ya kilimo, pia kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.



from MPEKUZI https://ift.tt/2ZlDkPU
via IFTTT

No comments:

Post a Comment