Friday, February 12, 2021

Urusi yasema iko tayari kuvunja mahusiano na Umoja wa Ulaya


Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema nchi yake iko tayari kuvunja uhusiano wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya ikiwa jumuiya hiyo itaiiwekea vikwazo vya kiuchumi. 

Kauli hiyo imetokana na vipande vya mahojiano yaliyochapishwa katika tovuti ya wizara hiyo ya Urusi hii leo ijumaa. 

Katika sehemu ya mahojiano hayo Lavrov amenukuliwa akisema kwamba Urusi haitaki kujitenga na ulimwengu lakini inajiandaa kwa hatua hiyo kwa sababu ikiwa mtu anataka amani basi anapaswa kujiandaa kwa vita.

Jana alhamisi wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba Umoja huo huenda ukaiwekea Urusi vikwazo vya usafiri na kuzia mali za washirika wa rais wa nchi hiyo Vladmir Putin ikiwezekana katika kipindi cha mwezi huu. 

Uhusiano baina ya Urusi na nchi za Magharibi unakabiliwa na shinikizo kubwa kwa mara nyingine kuhusiana na kitendo cha kukamatwa na kufungwa jela mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi Alexei Navalny.

-DW



from MPEKUZI https://ift.tt/3b2DvFh
via IFTTT

No comments:

Post a Comment