Thursday, March 4, 2021

Mawaziri Watatu Zanzibar Walioteuliwa na Rais Mwinyi Hivi Karibuni Waapishwa


Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewaapisha mawaziri watatu huku wao wakiahidi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta mabadiliko makubwa.
Walioapishwa leo Alhamisi Machi 4, 2021 Ikulu mjini Unguja, Zanzibar ni Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Omar Shaaban (Biashara na Maendeleo ya Viwanda) na  Nassor Ahmed Mazrui (Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto).

Mwingine aliyeapishwa ni kamishina wa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB), Salum Yussuf Ali.


from MPEKUZI https://ift.tt/3t1NrX5
via IFTTT

No comments:

Post a Comment