WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea na itayafanyia kazi malalamiko ya wabunge juu ya utaratibu wa ukaguzi unaofanywa kwenye mgodi wa Mererani,
“Nimesikia concern ya namna ukaguzi unavyoendelea pale katika mgodi wa Mirerani, nilipanga kutembelea Mirerani ili kuona hali hiyo na kutafuta ufumbuzi, nikuahidi Mhe. Spika na waheshimiwa wabunge kwamba tumepokea na Serikali tutalifanyia kazi,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 29, 2021) wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye ambaye alitaka maelezo juu ya utaratibu wa ukaguzi katika mgodi huo. Mbunge huyo alikuwa akichangia mjadala wa hotuba makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini.
Amesema Serikali inapata fedha nyingi kupitia madini ya Tanzanite yanayochimbwa katika mgodi huo hivyo haiwezi kushindwa kununua mtambo unaoweza kufanya ukaguzi wenyewe bila kusumbua mtu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
from MPEKUZI https://ift.tt/3gTNv8e
via IFTTT
No comments:
Post a Comment