NA TIGANYA VINCENT
Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 28.6 kwa ajili ya kuanza rasmi zoezi la kulipa fidia kwa wananchi wote ambao wamepisha ujenzi wa miundombinu ya bomba la mafuta ghafla la Afrika Mashariki,
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kwenye uzinduzi wa wa awali wa zoezi la ulipwaji fidia kwa wananchi uliofanyika Kitaifa katika Kijiji cha Sojo wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Alisema kwa upande wa Tanzania bomba hilo litatoka Kyaka mkoani Kagera hadi Chongoleni Mkoani Tanga.
Dkt Kalemani aliwahikisha wananchi wote ambao wamepisha ujenzi wa miundombinu ya bomba la mafuta ghafla la Afrika Mashariki watalipwa haki zao mapema kwa mujibu wa tathimini iliyofanyika.
Aidha Waziri huyo aliwataka Wakandarasi wanaojenga mradi kuanza kazi mara moja baada ya zoezi la fidia kuanza ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani aliwataka wakazi wote wa Mkoa huo ambao wameanza kupata fedha hizo kuzitumika kwa malengo yatakayowasaidia kupiga hatua kimaendeleo.
Alisema wakituma fedha hizo kinyume kwa malengo ya kujipatia maendeleo mara baada ya kuisha wasitegemee kutakuwa na fedha nyingine.
Balozi Dkt.Batilda aliongeza wakazi wa Tabora wakatumia mradi huo kama fursa mbalimbali kuwapatia maendeleo kupitia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya kuuza kwa wahandisi na wataalamu watakaotumika kujenga bomba hilo.
Aidha aliwataka wakazi wa maeneo ya mradi wanahikisha ulinzi wa vifaa vya utekelezaji wa mradi huo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania James Mataragio alisema zoezi la ulipaji fidia lipo tayari kuanza kwa maeneo yote 12 ambapo timu za Wawakilishi wa Serikali, Wawakilishi wa Kampuni ya EACOP,Kampuni ya Uthamini (White Night) na Kampuni ya Ushirikishaji na Kusaidia Jamii (JSB) zipo katika baadhi ya Mikoa yenye maeneo ya kipaumbele ya mradi.
Mkurugenzi Mkuu huyo alisema kwa kuanzia wataanza kulipa shilingi bilioni 2.5 katika maeneo ya vipaumbele na kisha kuendelea kwingine.
Alisema timu hizo zinafanya kazi za uhakiki wa wananchi waliopisha mradi,utoaji wa Elimu kwa wananchi waliopisha mradi,uhakiki wa Maeneo yatakayotumika kwa ujenzi wa makazi mbadala na utiaji wa saini wa mikataba ya fidia
Mataragio alisema mara baada ya kukamilika kwa taratibu jumla ya wananchi 391 waliopisha mradi watalipwa fidia
Aidha Mataragio alisema kwa wale ambao watafidiwa nyumba watakuwa tayari kuhamia kwenye makazi yao mapya kati ya miezi 6 hadi 12 kuanzia siku watakayolipwa fidia.
Alisema katika kipindi hicho cha kusibiria wananchi wanaopisha mradi watakuwa wamepangishiwa nyumba za kuishi kwa muda na Kampuni ya EACOP pamoja na kupata misaada ya ki-binadamu ikijumuisha chakula, mbegu za kisasa za Mazao na Mifugo, elimu na mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Ujasiriamali, kilimo na ufugaji.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika mashariki (EACOP) Martin Tiffen alisema watakahakikisha kaya zote zilizoguswa na mchakato wa utwaaji ardhi zinalipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo.
from MPEKUZI https://ift.tt/36kcoU3
via IFTTT
No comments:
Post a Comment