Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imefanikiwa kuokoa na kudhibiti Jumla ya Tsh . Milioni mia mbili kumi na tano ,laki sita na sitini elfu (215,660,000)/= ambazo zingepotea kwa kuchepushwa ,kufujwa ama kulipwa kwa watu wasiostahili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 2,2021 jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo ametaja mmoja wa uchepushaji ni gari la Ofisi ya katibu tawala mkoa wa Dodoma ambalo baada ya kupata ajali lilipelekwa kwenye gereji moja mkoani Dodoma na kubainika vifaa 101 vyenye thamani ya Tsh. Milioni themanini na Saba ,laki Saba na themanini na tano elfu(87,785,000/=) vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo.
"Tulishirikiana na wakala wa ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Dodoma ikabainika katika gari hilo kuna vifaa 101 vilichepushwa tuliingilia kati vifaa hivyo vikarejeshwa"amesema .
Bw. Kibwengo amesema kitendo cha uchepushaji ni kosa chini ya Sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2019 ambapo amewataka wamiliki wa gereji binafsi mkoani Dodoma kuacha mara Moja tabia ya wizi wa vipuri vya magari ya umma .
Aidha, Kibwengo amesema miradi 20 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni Moja ,milioni mia Saba sabini na tano laki Saba ,sitini na tatu elfu na mia Saba arobaini na sita (1,775,763,746/=) imekaguliwa katika sekta za elimu,Afya na ujenzi na kubaini uchepuzi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh. Milioni arobaini na Moja laki nane na hamsini elfu( 41,850,000/=) huku miradi 19 ikibainika kutekelezwa kwa kiwango stahiki.
Katika hatua nyingine Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU mkoa wa Dodoma imepokea taarifa 124 za malalamiko zikiwa ni taarika 52 pungufu ya zile zilizopokelewa kwa robo ya mwaka Jana ambapo taarifa zinazohusu rushwa ni 70 na 54 hazihusiani na rushwa .
Sekta zinazoongoza kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ni serikali za mitaa kwa asilimia 39,ardhi asilimia 19,sekta binafsi asilimia 7,elimu,Afya,na polisi kila Moja asilimia 6.
"Tumepokea taarifa 124 za malalamiko ambapo pia majalada 20 ya uchunguzi yalikamilika na mashauri mapya mawili yalifunguliwa Mahakamani na mashauri mawili yalitolewa maamuzi ambapo jamhuri ilishinda Moja na kushindwa Moja.
Sanjari na hayo Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema elimu imetolewa kwa makundi mbalimbali ya Kijamii wakiwemo Vijana na kufanya semina 28 ,mikutano 7 ya hadhara ,vipindi 11 vya redio,maonesho mawili na ufunguzi wa klabu 41 za wapinga rushwa na kusikiliza kero za rushwa Kupitia mpango wa TAKUKURU inayotembea.
Pia katika robo ya Julai,hadi Septemba ,2021 Kibwengo amesema wataweka msisitizo katika uelimishaji wakati wa mbio maalum za mwenge na kwa makundi hasa ya Vijana huku akitoa msisitizo ushiriki wa kila mwananchi katika mapambano dhidi ya rushwa.
from MPEKUZI https://ift.tt/3AkfEg0
via IFTTT
No comments:
Post a Comment