Na Mwandishi wetu- Dodoma
Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika kudhibiti mfumuko wa bei wa Taifa ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwezi June , 2021.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ruth Minja leo Julai 8, 2021 Jijini Dodoma ambapo amesema mfumuko huo kwa hapa nchini kwa mwezi Juni umefikia asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.3 mwezi Mei, Kenya 6.32 kutoka 5.87 ya mwezi Mei, 2021 na Uganda 2.0 kutoka 1.9 mwezi Mei, 2021 .
“Ongezeko dogo la Mfumuko wa Bei hapa nchini kwa mwaka unaoishia Mwezi Juni, 2021 unamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei na huduma kwa mwaka unaoishia mwezi Juni, 2021 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021 na kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania bado inafanya vizuri”, alisisitiza Minja
Akifafanua amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuchukua hatua za kudhibi mfumuko wa bei ili kuwawezesha wananchi kuendelea kuchangia katika kukuza uchumi na shughuli nyingine za maendeleo.
Baadhi ya bidhaa zilizoongezeka bei kwa mwezi June ni; vitambaa vya nguo kwa asilimia 8.5, nguo za wanawake kwa asilimia6.3, viatu vya wanawake kwa asilimia 6.3, viatu vya wanaume kwa asilimia 6.2, kodi ya pango asilimia 4.9, vyakula kwenye migahawa asilimia 5.6 na gharama za malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7
Kwa upande wa bei za vyakula na vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi June, 2021 umepungua hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka unaoishia mwezi Mei , 2021.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu Sura 351 na yenye mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na usambazaji wa Takwimu rasmi.
from MPEKUZI https://ift.tt/3hnLd16
via IFTTT
No comments:
Post a Comment