Wednesday, June 15, 2022

Watu Watatu wafariki ajali ya basi la Zuberi Shinyanga


Watu watatu wamefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Zuberi  kugonga kingo za daraja na kupinduka  eneo la Mwigumbi mkoani Shinyanga.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, George Kyando amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana Jumatano Juni 15, 2022 saa nane mchana katika barabara ya Mwanza-Shinyanga.

Amesema waliofariki ni pamoja na dereva wa basi hilo, Hamza Katima na kubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva kupata tatizo la afya akiwa safarini.



from MPEKUZI https://ift.tt/XCtgcqn
via IFTTT

No comments:

Post a Comment