Saturday, October 12, 2019

IGP Sirro Atoa ONYO Kwa Wanaojihusisha na ugaidi, ujangili na ujambazi...Asisitiza Ushirikiano na Nchi Jirani

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema ushirikiano wa nchi za Tanzania, Burundi Na DRC hasa kitengo cha ulinzi na usalama utamaliza matukio ya ugaidi na utekaji na kwamba hatua hii ni endelevu kwa nchi zote 3 kumaliza kabisa matukio ya kiuhalifu.

IGP Sirro amesema hayo katika kikao kazi cha usalama kwa Nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kilichofanyika Mkoani Kigoma kikiwa na lengo la kuimarisha usalama mipakani na kukabiliana na wahalifu kutoka Nchi hizo.

"Makosa ya ugaidi, ujangili, dawa za kulevya, ujambazi na biashara haramu ya kusafirisha binadamu huwezi kuishinda ukifanya kazi peke yako.

“Ni lazima upate ushirikiano kutoka nchi jirani unazopakana nazo. Ndio maana leo tunakutana na wenzetu wa Burundi kujadili na tutasaini mikataba ya ushirikiano baina ya vikosi vyetu vya polisi," alisema Sirro.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Burundi CPP Melchiade Ruceke ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa kinara wa kuchochea amani kwa Nchi hiyo na kubainisha kuwa watadumisha amani na kuibua wahalifu 

"Tutaendelea kuwakamata wahalifu wanaofanya ujambazi Tanzania na kukimbilia Burundi na pia nchi ya Tanzania itawakamata wale wanaoingia kutoka Burundi, tunataka amani katika nchi zetu," alisema Ruceke.


from MPEKUZI https://ift.tt/314Muyx
via IFTTT

No comments:

Post a Comment