Kampuni inayolenga kuleta mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watanzania, Tigo, leo imetangaza promosheni kabambe ijulikanayo kama Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo jijini Dodoma.Promosheni hiyo inaenda sambamba na msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako ambayo ilizinduliwa jijini Mwanza na itamalizika jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Tigo wanaoshiriki katika promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo kwa mara ya kwanza wana nafasi ya kushinda hadi Sh1 milioni kila wiki huku mshindi wa jumla ataweza kujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwid yenye thamani ya Sh23 milioni.
Washindi wa promosheni hiyo hutangazwa kila wiki na ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, wateja wanatakiwa kujisajili kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kwakutembelea tovuti www.tigomusic.co.tz nakuchagua neno ‘Trivia’.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Lilian Mwalongo alisema “Shindano hili ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kujumuika na kuungana na wateja wetu kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wa aina zote hapa nchini.”
Aidha, Mwalongo aliwajulisha wateja wa Tigo watakaoshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako jijini Dodoma kwamba wanaweza kulipia tiketi kwa njia ya Tigo Pesa kwa Sh5,000/= au pesa taslimu kwa Sh7,000.
“Kama kampuni inayolenga kuchochea matumizi ya digitali, tumejizatiti kutoa huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja kila siku.Ili kununua tiketi kupitia Tigo Pesa mteja anatakiwa kufuata hatua za kawaida za kutuma pesa na kutuma Sh 8,000/= kwenda namba 0678 888 888 na watapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo ya tiketi,” alisema.
Pia, aliwahimiza wateja wa Tigo walioko Dodoma kusajili upya namba zao za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole hasa wakati wa msimu huu wa Tigo Fiesta kabla ya mwezi Desemba.
Zoezi la kusajili namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole linalenga kudhibiti matumizi mabaya ya huduma za mawasilaino na pia kuwawezesha wateja kutambulika ili kupata hudma zenye usalama zaidi ikiwamo huduma za kifedha pamoja na malipo ya huduma kama maji, umeme pamoja na televisheni.
Mwisho.
from MPEKUZI https://ift.tt/2BcXijT
via IFTTT
No comments:
Post a Comment