Wanafunzi 39 wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Ihumilo kata ya Nkome Wilayani Geita wamenusurika kufa kwa radi wakati wakiwa darasani baada ya kupoteza fahamu kisha kukukimbizwa katika Hospital ya Wilaya Nzera na wengine Zahanati ya Nkome kwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 na mganga mkuu wa mkoa wa Geita, Josephat Simeo inaeleza kuwa wanafunzi 24 wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Nzera na 15 wamepatiwa matibabu katika zahanati ya Nkome.
Dk Simeo amesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza wanaendelea vizuri na tayari wanafunzi 36 wameruhusiwa kutoka hospitali.
Dk Simeo amesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza wanaendelea vizuri na tayari wanafunzi 36 wameruhusiwa kutoka hospitali.
from MPEKUZI https://ift.tt/2VSpFgv
via IFTTT
No comments:
Post a Comment