Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa hapo jana na Dkt. Mwinyi, zikiwa zimepita siku chache baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.
Hafla ya kuapishwa kwa Sharif imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Rais Dkt Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na chama cha ACT Wazalendo.
from MPEKUZI https://ift.tt/3kzGHN0
via IFTTT
No comments:
Post a Comment